Ndege ya Precision Air yapata ajali ziwani Bukoba, Shuhudia uokoaji ukiendelea

Ndege ya Shirika la Precision Air imepata ajali katika Ziwa Victoria, Bukoba mkoani Kagera. Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumapili 6, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amethibitisha taarifa za ajali hiyo na kusema kuwa yupo kwenye eneo la tukio akiendelea na uokoiaji. “Iko sahihi hiyo taarifa niko kwenye eneo la tukio nafanya uokozio, siwezi kuzingumza zaidi” amejibu kwa kifupi Kamnda Mwampaghale alipopigiwa simu. Video na picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha ndege hiyo ikiwa imetumbukia kwenye maji.
Back to Top