Balaa la mafuriko Kilimanjaro || Watu zaidi ya 4000 wakosa makazi ya kuishi

Watu zaidi ya 4000 katika eneo la kikavu chini kata ya Weruweru na Masama Mashariki Wilaya ya Hai,Mkoani Kilimanjaro hawana Makazi ya kuishi baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko yaliyotokana na kujaa kwa mto Namwi na kusababisha vifo vya watu watatu. Mafuriko hayo yalitokea Aprili 21 mwaka huu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani hapa na kusababisha kingo za mto huo kuvunjika na kupelekea kusombwa kwa gari lililokuwa limebeba watu watatu wa familia moja huku mwili wa mmoja umepatikana na jitihada za kutafuta miili ya watu wawili ikiendelea Leo kamati ya usalama ya Mkoa ilitembelea maeneo hayo ambayo yalivamiwa na maji Masama Mashariki,Kikavu chini na eneo la TPC ili kuangalia madhara yaliyosababishwa na mafuriko hayo. Akizungumza mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro,Anna Mghwira amesema madhara ni makubwa kutokana na kaya zaidi ya 700 zenye watu zaidi 4000 nyumba zao kuharibiwa na mafuriko hayo ambapo amesema serikali inaendelea na jitihada za kuona namna ya kuzisaidia kaya hizo.
Back to Top